OJADACT YAADHIMISHA SIKU YA KUPIGA VITA DAWA ZA KULEVYA NA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU
Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) kimeadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya na usafirishaji haramu, yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kutoa wito kwa waandishi wa habari kutumia vyema vyombo vyao kuielimisha jamii athari za dawa za kulevya.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Mganga Mkuu wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa, amesisitiza waandishi wa habari kuwa daraja la kuelimisha jamii juu ya athari za dawa.
Dkt. Rutachunzibwa pia ameishukuru OJADACT kwa kuandaa maadhimisho hayo kwa kuwaleta waandishi pamoja na kuwapitisha kwenye kujifunza athari za dawa za kulevya na kusema kitendo cha OJADCT kuwepo Mwanza kunasaidia kwenye mapambano ya dawa za kulevya.

Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo “tukabiliane na dawa za kulevya kwa ustawi wa jamii itumike kwenye kuielimisha jamii juu ya athari za dawa za kulevya nchini”.
Kwa upande wake mtoa mada Dkt. Eunice Masangu amesema kuwa, kwa sasa hospitali ya Mkoa ya Sekeouture inatoa huduma ya methadone kwa watumiaji wa dawa za kulevya za iroine kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) kinajikita kwenye mapambano ya dawa za kulevya nchini hivyo kila mwaka inaadhimisha siku hiyo.
Matuko katika PICHA wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya na usafirishaji haramu




