+255754551306 info@ojadact.org

Blog Details

Give a helping hand for poor people

Kalli: Waandishi andikeni habari zenye tija

Mkuu wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Salum Kalli ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kuandika habari zenye tija ili kuleta maendeleo ya taifa.

Kalli ametoa wito huo wakati akifungua maadhimisho siku ya Uhuru wa habar ngazi ya Mkoa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Internews Tanzania kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC) nakushikishisha waandishi wa habari kutoka mkoa wa Mwanza.

“Wananchi wanataka habari na habari zikiwa kamili na sisi kama serikali tutaendelea kuwaunga mkono waandishi wa habari,”amesema Kalli.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari wa Kupambana na Kupiga vita matumizi ya Dawa za Kulevya Tanzania (OJADACT) na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC) Edwin Soko ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kutumia vyema fursa ya ujio wa mitandao ya kijamii katika kuhabarisha umma.

“Ujio wa mitandao ya kijamii isitufanye kwenda kinyume na maadili yetu,niwasihi waandishi wenzangu kuandika habari kwa kuzingatia weledi na misingi ya taaluma,”amesema Soko.

Naye  Mratibu wa Programu kutoka taasisi isiyo ya kiserikali ya Internews Tanzania Shaban Ramadhan, amesema kuwa taasisi hiyo itaendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari nchini ili kuboresha maudhui pamoja na kuwawezesha waandishi wa habari kufika sehemu mbalimbali ambazo zimekuwa na ugumu kufikika.

Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa habari Duniania ufanyika Mei 3 ya kila mwaka kama sehemu ya kuenzi kazi, mafanikio, changamoto na madhira wanayo pitia waandishi wa habari kote ulimwenguni katika kazi zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

en_USEnglish