+255754551306 info@ojadact.org

Blog Details

Give a helping hand for poor people

Ushahidi kesi ya Zumaridi waanza kusikilizwa

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza imeanza kusikiliza ushahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili Diana Bundala maarufu kama ‘Mfalme Zumaridi’.

Katika kesi hiyo namba ya 11 ya mwaka 2022, Zumaridi na wafuasi wake nane wanakabiliwa na kesi ya kufanya shambulio la kuzuru mwili kwa Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Nyamagana, James Mgaya.

Akizungumza na vyombo vya habari Wakili wa utetezi, Erick Mutta amesema kuwa wameiomba mahakama hiyo kuita kesi hiyo mfululizo hili iweze kukamilika kwa wakati na haki kupatikana.

Aidha Wakili Mutta ameongeza kuwa, kuwahi kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo ni moja ya haki jinai za msingi katika utatibu wa kusikiliza mashauri.

Kesi hiyo ambayo inasikilizwa chini ya Hakimu Mkazi Monica Ndyekobora, imehairishwa hadi tarehe 19 May 2022 itakapo taja tena na washitakiwa wawili Zumaridi na Christina Mwisongo wakirudishwa rumande kutokana na kukosa dhamana.

Mwisho

Martin Nyoni

Mwanza- Tanzania

10 May 2022

Leave a Reply

Your email address will not be published.

en_USEnglish